Mpangilio Wa Kanda Za Usaili Wa Mahojiano Usaili Wa Mei Hadi Juni, 2025

Mpangilio Wa Kanda Za Usaili Wa Mahojiano Usaili Wa Mei Hadi Juni, 2025, Wasailiwa wote waliopangwa kushiriki usaili wa mahojiano kwa kipindi cha Mei hadi Juni 2025 wanasisitizwa kuzingatia mpangilio wa vituo vya usaili kama ulivyoainishwa hapa chini.

Kila msailiwa anatakiwa kufika katika Kanda ya Usaili wa Mahojiano kulingana na eneo alilofanyia usaili wa mchujo.

MPANGILIO WA KANDA ZA USAILI WA MAHOJIANO​

Na.Mahali/Mkoa wa Usaili wa MchujoKanda ya Usaili wa MahojianoKituo (Venue) cha Usaili wa Mahojiano
1Arusha, Manyara, Kilimanjaro, TangaArushaChuo cha Uhasibu Arusha (IAA)
2Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, PwaniDar es SalaamOfisi za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
3Dodoma, Iringa, Morogoro, SingidaDodomaOfisi za Sekretariati ya Ajira Katika Utumishi wa Umma – PSRS
4Mbeya, Njombe, Ruvuma, Songwe, RukwaMbeyaChuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)
5Geita, Kagera, Simiyu, Shinyanga, Mara, MwanzaMwanzaMwanza Alliance English Medium
6Katavi, Kigoma, TaboraTaboraShule ya Sekondari ya Wasichana – Tabora
7UngujaUngujaJengo la Katiba na Sheria – Mazizini

MAELEKEZO MUHIMU:

  • Wasailiwa wanaombwa kufika katika vituo vya usaili siku moja kabla ya siku ya mahojiano.
  • Wajitahidi kuwa na vitambulisho halali na nyaraka zote muhimu kama zilivyoelekezwa katika barua ya kuitwa kwenye usaili.
  • Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti rasmi ya Sekretariati ya Ajira:www.ajira.go.tz

MPANGILIO WA KANDA ZA USAILI WA MAHOJIANO MEI HADI JUNI 2025-1 PDF
 
Back
Top