Uni Jamii

Habari Ndugu, Ili Kuendelea kufaidika na Taarifa zeru Muhimu , karibu ujisajili!

Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2025

Assa

New member
Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2025 | Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya NECTA Kidato Cha Sita

Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita (NECTA) ni moja kati ya matokeo muhimu katika safari ya elimu ya kila mwanafunzi nchini Tanzania. Matokeo haya huchangia kwa kiasi kikubwa mwenendo wa wanafunzi nchini kwasababu ndio hutumika kama kigezo cha kujiunga na elimu ya ngazi ya juu kama vile elimu ya shahada na astashahaada. Pia Matokeo ya NECTA kidato cha sita hutumia na baadhi ya makampuni na tasisi katika kuajiri wafanyakazi wa nafasi mbalimbali.

Wakati wanafunzi, wazazi, walezi, na walimu wote wanasubiri kwa hamu kubwa zoezi la kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita na Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) ni muhimu kuwa na taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu jinsi ya kuangalia matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita 2025. Mwongozo huu wa kina umetayarishwa kwa lengo la kuwapa wanafunzi, wazazi, walezi, na walimu taarifa zote muhimu ili kuhakikisha wanapata matokeo yao kwa urahisi na bila usumbufu.

Mwongozo huu utaelezea kwa undani njia mbalimbali ambazo wanafunzi wanaweza kutumia kuangalia matokeo yao, ikiwa ni pamoja na kuangalia kupitia mtandao, ujumbe mfupi wa simu (SMS), au moja kwa moja shuleni. Aidha, mwongozo huu utawapa vidokezo muhimu vya kuzingatia kabla na baada ya kuangalia matokeo, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kujiandaa na nini cha kufanya baada ya kupokea matokeo.

Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2025​


Katika kipindi hiki cha kusubiri kwa matokeo ya Kidato cha Sita 2025, NECTA imejitahidi kurahisisha upatikanaji wa matokeo kuanzisha njia mbalimbali za kuangalia. Wanafunzi, wazazi, na wadau wote wa elimu sasa wanaweza kutumia njia hizi kupata taarifa muhimu kuhusu matokeo haya kwa haraka na urahisi. Ufuatao ni muhtasari wa njia hizo zitakazowawezesha kuangalia matokeo ya Kidato cha Sita 2025.

  1. Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Sita Mtandaoni (Online)
  2. Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita Kupitia USSD
  3. Kuangalia Matokeo ya NECTA Kidato cha Sita Mashuleni

Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 Kupitia Mtandao (Online)​


Njia rahisi na inayopendelewa na wengi ni kuangalia matokeo ya Kidato cha Sita 2025 kupitia mtandao. Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) hutoa matokeo haya kwenye tovuti yao rasmi. Ili kuangalia matokeo yako, fuata hatua zifuatazo:

  1. Tembelea tovuti ya NECTA: Fungua kivinjari chako cha intaneti (kama vile Google Chrome, Mozilla Firefox, au Safari) na uandike anwani ya tovuti ya NECTA (www.necta.go.tz) kwenye kisanduku cha anwani. Kisha, bonyeza “Enter” ili kuingia kwenye tovuti.
  2. Nenda kwenye menyu ya matokeo: Kwenye ukurasa wa nyumbani wa tovuti ya NECTA, tafuta sehemu iliyoandikwa “Results”. Bonyeza sehemu hiyo ili kuendelea.
  3. Chagua Matokeo ya ACSEE: Katika ukurasa wa matokeo, utaona chaguo mbalimbali za mitihani. Chagua “Matokeo ya ACSEE” ili kuonyesha matokeo ya Kidato cha Sita.
  4. Chagua mwaka wa matokeo: Baada ya kuchagua “Matokeo ya ACSEE,” utaona chaguo la miaka tofauti ya mitihani. Chagua “Matokeo ya ACSEE 2025” ili kuona matokeo ya mwaka 2025 pekee.
  5. Tafuta shule yako: Kwenye ukurasa unaofuata, utaona orodha ya shule zote zilizofanya mtihani wa Kidato cha Sita. Tumia kisanduku cha kutafutia (search box) ili kuandika jina la shule yako na ubofye “Enter” au “Search.”
  6. Fungua kiungo cha shule yako: Baada ya kupata jina la shule yako, bonyeza kiungo chake ili kuona matokeo ya wanafunzi wa shule hiyo.
  7. Tafuta jina lako: Kwenye ukurasa wa matokeo ya shule yako, tafuta jina lako kwa makini.

Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2025

Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2025

Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita Kupitia USSD


Kwa wale ambao hawana urahisi wa kutumia intaneti, NECTA imetoa njia ya kuangalia matokeo kupitia SMS. Njia hii ni rahisi na ya haraka, na inahitaji tu kuwa na simu ya mkononi yenye uwezo wa kutuma na kupokea ujumbe mfupi. Ili kuangalia matokeo yako kupitia SMS, fuata hatua zifuatazo:

  1. Piga *152*00#: Fungua sehemu ya kupiga simu kwenye simu yako na piga namba *152*00#. Kisha utaona orodha ya huduma mbalimbali kwenye skrini ya simu yako.
  2. Chagua Elimu: Kutoka kwenye orodha, chagua namba 8 (ELIMU) kwa kutumia vitufe vya simu yako.
  3. Chagua NECTA: Baada ya kuchagua “Elimu,” utaona orodha nyingine ya huduma. Chagua namba 2 (NECTA).
  4. Chagua Matokeo: Kwenye orodha inayofuata, chagua namba 1 (MATOKEO).
  5. Chagua ACSEE: Utaona orodha ya aina za mitihani. Chagua namba 2 (ACSEE) kwa kuwa unataka kuangalia matokeo ya Kidato cha Sita.
  6. Andika namba ya mtihani na mwaka: Sasa, andika namba yako ya mtihani (index number) pamoja na mwaka wa mtihani. Kwa mfano, kama namba yako ya mtihani ni S0334-0556 na mwaka wa mtihani ni 2025, andika S033405562025.
  7. Chagua aina ya malipo: Utaombwa kuchagua jinsi ya kulipa gharama ya huduma hii. Kawaida, gharama huwa ni Tshs 100/= kwa kila SMS. Chagua njia ya malipo inayokufaa zaidi.
  8. Pokea matokeo: Baada ya kukamilisha malipo, utapokea ujumbe mfupi (SMS) wenye matokeo yako ya Kidato cha Sita 2025.

Kuangalia Matokeo ya NECTA Kidato cha Sita Mashuleni


Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2025 Shuleni


Shule nyingi nchini Tanzania hupokea matokeo ya wanafunzi wao moja kwa moja kutoka NECTA na kuyabandika kwenye ubao wa matangazo wa shule. Wanafunzi wanaweza kutembelea shule zao ili kuangalia matokeo yao kwenye ubao huu.

Aidha, walimu wakuu, walimu wa darasa, au maafisa wengine wa shule wanaweza kutoa msaada kwa wanafunzi ambao wanakabiliwa na changamoto zozote katika kuangalia matokeo yao ya mtihani wa kidato cha sita 2025. Ni muhimu kwa wanafunzi kuwasiliana na shule zao mapema ili kujua utaratibu maalum wa kuangalia matokeo shuleni.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top